Kumekuwa na mjadala
unatembea mitandaoni kuhusiana na Haji Manara kuangua kilio mahakamani Kisutu,
jana.
Manara ambaye ni
msemaji wa Simba, aliangua kilio baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu
wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kutakiwa kwenda mahabusu baada ya kusomewa
mashitaka ya utakatishaji fedha.
Suala hilo lilionyesha
kumuumiza Manara ambaye alitafuta sehemu akakaa na kuangua kilio hasa baada ya
kusikia wanakwenda mahabusu hadi Julai 13, kesi yao itakaposikilizwa leo.
Katika makundi
mbalimbali ya Whatsapp ambayo yanahusisha Yanga au Simba, wengi wamekuwa
wakimuonea huruma Manara kutokana na picha zinazomuonyesha akiangua kilio.
Wengine
wamekuwa wakimtania kutokana na utani wa Yanga na Simba lakini asilimia kubwa
wakimpa moyo kutokana na matatizo yanayowakabiri.
EmoticonEmoticon