Thursday, 22 June 2017

Muller amuondosha mashindano Wilfried Tsonga

Tags


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
 Jo Wilfried Tsonga wa upande wa kulia akimpongeza Gilles Muller baada ya mchezo kumalizika

Mfaransa Jo-Wilfried Tsonga ameondolewa kwenye michuano ya Aegon, inayoendelea nchini England na Gilles Muller kutoka Luxembourg
Muller hana jina kubwa katika ramani ya mchezo wa tenesi alimfunga Tsonga kwa seti mbili katika raundi ya pili ya mchuano wao.
Katika seti ya kwanza Muller alishinda kwa 6-4 na seti ya pili akishinda kwa 6-4.
Tsonga anakua nyota wa nne kutupwa nje ya mashindano hayo baada ya Andy Murray, Stan Wawrinka na Milos Raonic kuondolewa hapo siku ya jumanne .


EmoticonEmoticon