KIUNGO Thaban
Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma wametuliza mzuka baada ya kuwaambia
mabosi wa Yanga kwamba wapo tayari kubaki kwa muda zaidi katika kikosi hicho.
Taarifa zilizoifikia saluti5 zimesemsema Kamusoko amesema anakuja nchini wiki
hii kumalizana na Yanga baada ya mafanikio katika mazungumzo ya kuongeza
mkataba zaidi. Kiungo huyo fundi amesema anataka kubaki Yanga ambayo imempa
heshima kubwa hasa baada ya hivi karibuni kurejeshwa katika kikosi cha taifa na
kwamba haoni kama watashindwa katika mazungumzo ya mwisho yatakayofanyika hapa
nchini mara baada ya kuwasili.
“Nitakuja hapo Tanzania wiki hii,
nimeshazungumza na viongozi na tuko katika sehemu nzuri. Wana Yanga wasiwe na
wasiwasi, hakuna kitakachoshindikana,” alisema Kamusoko. Wakati Kamusoko
akiyasema hayo, mmoja wa mabosi wa usajili, amesema Ngoma amekubali kusaini
mkataba mpya wa kubaki ambapo hatma yake nae itajulikana mara baada ya
kuwasili.
Ngoma ambaye kwa sasa yuko kwao Zimbabwe kwa mapumziko, inaelezwa
kiasi cha dola 40,000 kitatumika katika kumuongezea mkataba huo ambapo utakuwa
mkataba wa pili kwake na Yanga.

EmoticonEmoticon