Ile ndoto ya kiungo wa
Yanga, Simon Happygod Msuva ya kutaka kucheza soka la kulipwa nje ya nchi,
inaweza kukamilika sasa baada ya uongozi wa timu hiyo kuweka wazi kuwa maongezi
baina yao na timu ya Difaa El Jadida ya Morocco yamefikia kwenye hatua nzuri.
WAMOROCCO hao
wanaiwinda kwa udi na uvumba saini ya Msuva aliyefunga mabao 14 katika msimu
uliopita ambapo awali walikuwa tayari kumlipa dola 4,000 (karibu milioni tisa)
kama sehemu ya mshahara wake.
Kaimu Mkuu wa Kitendo
cha Habari cha Yanga, Godlisten Anderson ‘Chicharito’, amesema kuwa wao kama
uongozi wa Yanga wanaendelea ambapo kuna asilimia 85 za Msuva kuondoka ndani ya
kikosi hicho.
“Ndani ya muda mfupi
kila kitu kuhusiana na suala la Msuva kwenda Morocco kitakuwa wazi ambapo kwa
sasa viongozi wanaendelea kulishughulikia kuhakikisha Msuva anaenda kukipiga
nchini humo.
“Kuna asilimia 85 ya
yeye kuondoka na tayari tumeshawaandaa baadhi ya wachezaji kuziba pengo lake
pale atakapoondoka ambapo kuna wachezaji kama Juma Mahadhi wanaweza kuziba
nafasi yake pale atapoondoka,” alisema Chicharito.
Msuva kwa sasa
amebakisha mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuendelea kuitumikia Yanga ambayo
inanolewa na Mzambia, George Lwandamina.

EmoticonEmoticon