CHELSEA inakaribia kushinda mbio za kuwania saini ya kiungo
wa ulinzi wa Monaco, Tiemoue Bakayoko.
Gazeti la Daily Mail limedai kwamba
uhamisho wa kiungo huyo utaigharimu klabu hiyo bingwa wa Premier League pauni
milioni 35 baada ya Antonio Conte kuweka wazi kuwa anamtaka Stamford Bridge
staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Chelsea tayari imeshakubaliana na Monaco
juu ya ada ya kiungo huyo ambaye atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na
mabingwa hao wa England katika dirisha hili la kiangazi.
Bakayoko pia alikuwa
akitakiwa na Manchester United na Arsenal, lakini ripoti kutoka Ufaransa
zimedai kuwa kiungo huyo wa miaka 22 ameonyesha nia ya kutaka kufanya kazi
chini ya Conte.

EmoticonEmoticon