INAWEZA kuwa ni habari mbaya kwa wapenzi wa FC Barcelona
duniani kote. Habari yenyewe ni kwamba mwanasoka mwenye mvuto kuliko wote
katika kikosi chao, Neymar Jr anajiandaa kuhamia kwa mahasimu wao wakubwa, Real
Madrid.
Gazeti moja nchini Hispania limeandika kwamba mwanasoka huyo raia wa
Brazil anakamilisha mipango ya kuhamia Real Madrid kutokana na kuchoshwa na
mambo yanavyokwenda katika kikosi cha Barcelona. “Neymar kuna wakati alikuwa
ahamie kwetu, lakini mambo hayakuwa kama tulivyotaka.
Lakini sasa tunamtaka
tena,” amesema rais wa Real Madrid, Florentino Perez. Hata hivyo, amesema
kwamba sasa anaona kwamba kuna nafasi ya kumvuta tena kwao. “Anaweza kuhamia
Real Madrid na wakati mwafaka utafika. Sina hakika kama kuna makubaliano yoyote
kati yake na klabu yake,” limeandika gazeti hilo.
Perez amesema itakuwa jambo
la maana kabisa kama mwanasoka huyo nyota atahamia kwenye kikosi chao.
Mwanasoka huyo wa Brazil alijiunga na Barcelona mwaka 2013 na alitengeneza
pacha kubwa kati yake na washambuliaji wawili; Lionel Messi na Luis Suarez.
Hata hivyo, imedaiwa kuwa mwanasoka huyo atahamia Real Madrid kama cristiano
Ronaldo ataondoka kwenye kikosi hicho. Ronaldo amekuwa akihusishwa na kuondoka
katika kikosi hicho kufuatia kili alichosema kwamba hajapewa ushirikiano na
klabu hiyo katika madhira ya kodi yanayomhusu.
“Neymar alifaulu mpaka vipimo
vya afya katika Madrid. Tulijaribu kumleta hapa wakati fulani lakini tukaachana
na ile mipango,” alisema Perez akiongea na radio moja ya nchini Hispania, Onda
Cero.

EmoticonEmoticon