KIPA wa Liverpool Loris Karius amesema kwamba ingawa katika
kikosi chake kuna changamoto nyingi, lakini anajua ataendelea kudaka. Akiongea
juzi kipa huyo wa zamani wa klabu ya Ligi Kuu ya Ujerumani ya Mainz amesema
kwamba pamoja na changamoto nyingi ambazo zinamkabili lakini anataka kubaki
kuwa kipa namba moja katika kikosi hicho cha klabu ya Merseyside.
Wakala wa
mchezaji huyo, Florian Goll amesema habari kwamba mchezaji wake anataka kurudi
Ujerumani ni za uongo. Wakala huyo amesema kwamba anajua kuwa mchezaji huyo ana
changamoto kubwa kutoka kwa kipa mwingine, Simon Mignolet lakini mawazo yake ni
kwamba atabaki Liverpool.
Amesema kwamba Karius ni kipa mzuri lakini pamoja na
mwenzake Simon Mignolet wanatakiwa kupambana kwa ajili ya Liverpool. Karius
ambaye amepoteza kuwa kipa namba moja wa kikosi hicho, amekuwa akitajwa kwamba
anataka kurudi Ujerumani, lakini wakala wake amesema kwamba kipa huyo atabaki
Liverpool.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa hajawahi kukosa imani
na kipa huyo na kwamba ikiwa yeye mwenyewe anataka kurejea Ujerumani, hiyo ni
habari nyingine. “Sina hakika kama anataka kuachana na Liverpool, lakini kwa
upande wangu sijawahi kukosa imani nae. Ndio, kuna wakati kipa lazima apoteze
namba kwa mpinzani wake, lakini haina maana kwamba kipa huyo sio bora,” amesema
Klopp

EmoticonEmoticon