MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Chile anayekipiga katika klabu
ya Arsenal ya Uingereza, Alexis Sanchez anatajwa kuwa amekubali kujiunga na
klabu ya Manchester City. Mwandishi mmoja wa habari ambaye ni rafiki mkubwa wa
mwanasoka huyo amesema jana kwamba ameambiwa “laivu” na Sanchez kwamba
anaondoka rasmi na chaguo lake ni Manchester City.
Gerard
Romero ambaye ni mwandishi wa habari raia wa Hispania amesema kwamba ameambiwa
na sanchez kwamba anakwenda Man City ili kuungana na kocha wakw wa zamani Pep
Guardiola. Arsenal imekuwa kwa muda mrefu sasa ikihaha kumbakiza mchezaji huyo
katika kikosi chake, lakini kwa tarifa hizo mpya ni kama vile jitihada hizo
zimekwama.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na msimu bora katika
Arsenal chini ya kocha wake, Arsene Wenger na ametumbukiza kambani mabao 30
katika mechi zote za mashindano. Hata hivyo, winga huyo yuko nje ya mkataba
msimu ujao na kama anaondoka kwenda Man City maana yake anaondoka akiwa kama
mchezaji huru.
Na kwa mujibu wa Romero, tayari mazungumzo ya uhamisho wake
yanaweza kuanza wakati wowote ili kujua ni kiasi gani arsenal inaweza kumpa
kutokana na muda mdogo wa mkataba wake uliobaki. Mwandishi huyo ameandika
kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Alexis Sanchez amekamilisha uhamisho wake
kwenda man City. Manchester na Arsenal wameridhia uhamisho wake.
” Wiki
iliyopita Sanchez ameiambia Arsenal kwamba hana haraka ya kujadili kuhusu
mkataba mpya mpaka baada ya mashindano ya Kombe la mabara. Pep Guardiola
amekuwa katika mawindo makali ya kusaka wachezaji wa maana kwa ajili ya
kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao.

EmoticonEmoticon